Search This Blog

TANZANITE CITY: The Africa's Factory & Innovation Powerhouse!

TANZANITE CITY: The Africa's Factory & Innovation Powerhouse!
We Will Turn Bushes Into Highly Industrialized City

Sunday, October 22, 2017

Tanzanite City Part 02: Tuliyojifunza Toka Kwa Wengine!

Wazo la kuanzishwa kwa Tanzanite City limetokana na tafiti nyingi tulizozifanya kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi iliyopita. Tafiti hizo zililenga kutufanya tujue wenzetu waliokuwa na ndoto kama zetu walipitia changamoto zipi, na kama waliweza kufaulu walifanya nini cha tofauti na kama walifeli walikosea wapi. Vilevile tulilenga kutambua mifumo na mikakati sahihi ya kufuata ili kuweza kuwa na mafanikio tunayohitaji kuifikia Tanzania ya viwanda. Mambo yafuatayo tuliyazingatia kwenye tafiti zetu:
a.     Tuliangalia matarajio na mwenendo wa masuala ya teknolojia na ubunifu pamoja na mabadiliko katika uchumi wa dunia
b.     Historia na uzoefu wetu hapa nyumbani na wa mataifa mengine katika masuala ya sayansi na teknolojia pamoja na maendeleo ya kitaasisi.
c.     Tuliangalia hali halisi ya sasa, uwezo na rasilimali tulizonazo, miundo ya kitaasisi na mikakati yetu kama taifa
d.     Tukafanya upembuzi wa mafanikio na matatizo/changamoto ambazo mataifa mengine yaliyokuwa na malengo kama yetu walipitia katika kufikia malengo yao.
Tafiti hizo zilituonyesha kuwa, iwapo tutatengeneza mazingira hamasishi kwa shughuli za utafiti na ubunifu pamoja na kuwezesha uanzishaji wa makampuni kwa utaratibu rahisi na rafiki kisha kuwavutia wawekezaji wa nje kuingia ubia na watanzania, Tanzania inaweza kabisa kupiga hatua kubwa katika mapinduzi ya teknolojia na viwanda sawa kabisa na mataifa mengine yote yaliyoendelea ikiwamo Uchina, india, Indonesia, Malaysia n.k.
Kwa hiyo mchakato wa ujenzi wa Tanzanite city unatokana na uzoefu tulioupata kutoka kwa mataifa ambayo yamefanikiwa kupata maendeleo makubwa ya kiteknolojia na kiviwanda katika miongo michache iliyopita. Swala la msingi ni kuhakikisha kuwa mchakato mzima unaendana na hali halisi na changamoto mahsusi za taifa letu na mazingira yaliyopo. Vile vile, mchakato mzima lazima ujikite katika mipango halisi na inayotekelezeka.
Ili kuweza kukidhi mahitaji ya kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa viwanda, uanzishwaji wa jiji la Tanzanite City umezingatia mambo yafuatayo ambayo ni ya msingi:
a.    Mkakati mahususi (Focused strategy); mkakati mahsusi wa ujenzi wa Tanzanite City ni kujenga na kuimarisha uwezo wetu wa ndani wa kubuni teknolojia na kuanzisha viwanda pamoja na makampuni ya teknolojia. Kuwashirikisha watanzania wazawa kupitia klabu ya marafiki wa Tanzanite City kumiliki viwanda na makampuni badala ya kubaki watazamaji tu ndani ya nchi yao.
b.    Miundombinu inayokidhi haja maridhawa (Sound facilities & infrastructures); ujenzi wa miundombinu muhimu utawanufaisha wanasayansi na wabunifu wetu kwa kuwawezesha kufanya tafiti zao kwa uhakika na kujiamini.
c.     Kujenga mfumo madhubuti wa biashara (Adequate business systems); mfumo madhubuti wa kibiashara utarahisisha upatikanaji wa huduma muhimu na kuvutia wawekezaji, wafanyabiashara na wajasilamali pamoja na wataalam mbalimbali katika fani zote kuja kuwekeza rasilimali zao Tanzanite City.
d.    Ukuzaji wa teknolojia na vipaji (Development of talents and technology); kukuza vipaji na uendelezaji wa teknolojia kwa kuwajengea uwezo vijana wanaomaliza katika taasisi zetu za elimu ya juu na kuwawezesha kubuni teknolojia na vifaa vya uzalishaji pamoja na kuwasaidia kujenga viwanda na kuanzisha makampuni.
e.    Kuwezesha upatikanaji wa mitaji na fedha (Access to capital and financing); moja ya matatizo makubwa ya wajasiliamali na wataalam wa teknolojia hapa nchini ni upatikanaji mgumu wa mitaji na fedha za kugharimia tafiti na kubunifu. Tanzanite City ina mkakati wa makusudi wa kuhakikisha kuna upatikanaji wa uhakika wa fedha za mitaji na kuendeshea tafiti mbalimbali. Lengo ni kuwafanya wataalam wetu wazingatie zaidi shughuli za kitafiti badala ya kufikiria namna ya kupata pesa kwa ajili ya kuendesha maisha pamoja na kujikimu wao wenyewe.
f.      Kusaidia kupromoti taasisi za wajasiliamali na ujasiliamali (Promotion of SMIEs and entrepreneurship); baada ya wataalam wetu kubuni teknlolojia na bidhaa zao kwa ufanisi, kujenga uwezo wa kuzalisha kwa wingi na kwa viwango vya kimataifa, kitakachofuata ni kuwasaidia kujenga viwanda na kuanzisha makampuni watakayo yamiliki kwa ubia na watanzania wengine kupitia klabu ya marafiki wa Tanzanite City. Makampuni haya ndiyo yatakayo tengeneza fursa za kibiashara ambazo ndizo zitakazowaletea fedha pamoja na kujenga  mahusiano baina ya watanzania na wawekezaji wa kigeni katika masuala ya teknlolojia na viwanda
MTANZANIA MWENZANGU UKIONA JAMBO HALIJAFANYIKA, JUA NI MIMI NA WEWE HATUJALIFANYA. ACHA LAWAMA NA UCHUKUE HATUA; JIUNGE NA KLABU YA MARAFIKI WA TANZANITE CITY USHIRIKI KUIJENGA TANZANIA MPYA YA VIWANDA KUPITIA TANZANITE CITY!
Kwa maelezo zaidi tembelea - https://esta-tanzanitecity.blogspot.com/p/friends-club-of-tanzanite-city.html
Katika sehemu itakayofuata (Tanzanite City - Part 03) tutazungumzia Klabu ya Marafiki wa Tanzanite City; nini lengo la kuanzishwa kwake, kwa nini ni muhimu ujiunge na klabu, fursa na faida za kuwa mwanachama au rafiki wa Tanzanite city n.k.  TWENDE PAMOJA HADI KIELEWEKE!

No comments:

Post a Comment