Mpango wa ujenzi wa jiji la sayansi, teknolojia na
ubunifu katika wilaya ya Chunya mkoani
Mbeya unatoa fursa nyingine ya kiuchumi kwa watanzania na wakaazi wa mkoa wa
Mbeya. Katika wakati ambapo nchi yetu
ipo kwenye kipindi cha mpito kuelekea uchumi wa kati na wa viwanda, mkoa wa
Mbeya chini ya uongozi wa Mh. Amosi Makalla kwa kushirikiana kampuni ya ESTA-TZ
na uongozi mzima wa wilaya na halmashauri ya wilaya ya Chunya umeanzisha mpango
maalum wa kuifanya Mbeya kuwa kitovu cha maendeleo ya teknolojia na mapinduzi ya
viwanda katika bara letu la Africa kusini mwa jangwa la sahara.
Katika mpango huu ambao eneo la kuanzia, kiasi cha
kilomita za mraba miatano (500sqKm) katika wilaya ya Chunya, litatumika kujenga
jiji la Tanzanite. Lengo kuu likiwa ni kuondoa utegemezi wa taifa letu kwa
bidhaa na teknolojia mabalilmbali toka nje ya nchi. Katika kipindi cha miaka
kumi na tano ijayo Tanzanite city inatarajiwa kujenga uwezo wa taifa letu
katika ubunifu wa teknolojia na uzalishaji wa viwandani.
Ili kufikia lengo ambalo mkoa wa Mbeya umejiwekea kufikia
mwaka 2030, mkakati mahsusi umewekwa wa kuwekeza kwa Vijana wenye vipaji
wanaohitimu kutoka katika taasisi zetu za elimu ya juu. Pindi wanapohitimu masomo yao, Vijana hao watakuwa
wanawekwa kwenye makambi maalumu ya teknlolojia ndani ya jiji la Tanzanite,
ambako huko watapewa kila kitu wanachohitaji kuweza kujenge uwezo katika
masuala ya ubunifu wa teknolojia na uzalishaji. Vijana hawa watakuwa wanapatiwa
mafunzo maalumu ya kuwawezesha kuanzisha na kuendeleza viwanda vitakavyotokana
na kazi za kibunifu watakazokuwa wanazifanya makambini.
Mpango huu utawawezesha wazawa wote bila kujali mazingira
wanayotoka au asili ya mtu, kuweza kumiliki viwanda kwa pamoja na vijana
wabunifu ambao ndiyo watakuwa wakurugenzi wa makampuni hayo yatakayoundwa. Hadi
sasa kuna maeneo zaidi ya mia tatu (300 Technology development missions) ambayo
yapo tayari kuanza kufanyiwa kazi na vijana pindi ujenzi wa awali wa miundo
mbinu muhimu utakapokamilika. Inatarajiwa kwamba maandalizi ya awali ya ujenzi
wa Tanzanite City yatakamilika mwishoni mwa robo ya kwanza mwakani (March 2018)
ambapo jiji litaanza rasmi shughuli zake.
Miezi sita baadaye viwanda visivyopungua 60 vitaanzishwa
na kutoa ajira za moja kwa moja kiasi cha 1200. Baada ya hapo kila wiki
kutakuwa na viwanda vipya vinaanzishwa na idadi yake itakuwa ikiongezeka siku
hadi siku ambapo katika miaka 15 hadi 2030 jumla makmpuni 54,600 yanatarajiwa kuanzishwa na kutoa ajira
za moja kwa moja zisozopungua milioni mbili na nusu.
Tafiti zinaonyesha kuwa kila ajira moja rasmi inazalisha
ajira kati ya tatu hadi tano zisizokuwa rasmi. Hivyo katika kipindi cha miaka
kumi na tano ijayo Tanzanite City itaweza kuzalisha ajira kwa watu wanaokaribia
milioni saba. Sehemu kubwa ya watu hawa pamoja na familia zao watakuwa wanaishi
ndani ya wilaya ya Chunya na maeneo jirani katika mikoa ya Songwe na Mbeya. Idadi
hii ya watu itahitaji miundombinu mbalimbali ambayo Tanzanite City imejiandaa
kikamilifu kuijenga kwa kushirikiana na marafiki pamoja na wadau wetu wote wa
maendeleo katika mkoa wa Mbeya.
Tanzanite City inaleta fursa ya kipekee kwa wakazi wa Mbeya,
na watanzania wote kwa ujumla, kwani kupitia klabu ya marafiki wa Tanzanite
City kila mwanzanchi Mtanzania ataweza kushiriki kwa namna moja au nyingine
katika kujenga uchumi wa viwanda. Lakini pia kupitia klabu ya marafiki wa
Tanzanite City, watoto wa watanzania masikini wataweza kupata fursa ya kutumia
vipaji vyao kubuni teknolojia na kuanzisha makampuni watakayoyamiliki kwa
pamoja na watanzania wengine ambao pia ni wanachama wa klabu. Jambo hili
lisingewezekana bila ya Tanzanite City. Kwa utaratibu huu hakuna mtanzania
atakayeachwa nje ya uchumi wa viwanda kama atakuwa mwanachama wa klabu isipokuwa
kwa mapenzi yake mwenyewe!
Klabu ya marafiki wa Tanzanite City ni chombo muhimu sana
kwa ujenzi wa jiji la Tanzanite na uchumi wa viwanda kama tunavyotaka kwa
sababu kuu mbilli; moja ni kuwa, klabu ndiyo njia pekee ya uhakika
itakayowaunganisha watanzania wote na kuwapatia fursa ya kushiriki kikamilifu
katika ujenzi wa Tanzania ya viwanda kama wadau na wamiliki. Pili, klabu
kupitia michango na ada za wanachama ni chanzo muhimu cha mapato
yatakayowezesha kugharimia shughuli na miradi mbalimbali ya ujenzi wa jiji na
uendelezaji teknolojia. Wananchi kupitia klabu watafaidika na fursa nyingi sana
zitakazotokana na ujenzi wa jiji hili hasa katika maeneo ya miundombinu, na
huduma.
Kwa kuzingatia kuwa jiji la Tanzanite litakuwa kiwanda na
kitovu cha mapinduzi ya viwanda na maendeleo ya teknlojia katika ukanda huu wa
maziwa makuu ya Afrika, watu kutoka mataifa mbalimbali ya afrika watakuja Mbeya
aidha kama watalii, wawekezaji ama wafanya biashara, hivyo kupelekea kuwa na fursa
nyingi sana, baadhi nimeziorodhesha hapa:
1.
Huduma;
Usafiri na usafirishaji
wa watu na mizigo, huduma za hoteli na mikahawa, huduma za afya, elimu ya
msingi, secondary na vyuo (mahitaji ya vyuo ni makubwa kiasi cha kuhitajika
vyuo zaidi 16 vitavyo toa kozi maalumu zinazoendana na mahitaji ya shughuli za
Tanzanite City), ukusanyaji wa taka ngumu, huduma za ulinzi na usalama, huduma za
simu na data, n.k.
2.
Miundombinu
Ujenzi wa
barabara, mitandao ya maji safi na maji taka, uzalishaji na usambazaji wa umeme,
mawasiliano, n.k.
3.
Ujenzi wa nyumba
Nyumba za
kuishi, majengo ya biashara, ofisi na viwanda
4.
Biashara
Bima, mabenki,
maduka makubwa (Malls), wasambazaji wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya jiji, wauzaji
wa bidhaa kwa matumizi ya nyumbani kama vyakula na vifaa vingine, sehemu za
burudani, n.k.
Ili mtu aweze kunufaika na fursa hizo, ni sharti awe
mwanachama wa klabu ya marafiki wa Tanzanite City, kwa maana nyingine anatakiwa
kuwa RAFIKI wa Tanzanite City. Rafiki wa kweli ni mtu ambaye yupo tayari
kujitoa kwa kila hali kwa ajili ya manufaa ya rafiki yake hata kama yeye
mwenyewe hafaidiki moja kwa moja na kujitoa huko. Marafiki wa Tanzaite City
watakuwa tayari kuichangia Tanzanite City kwa kulipia ada zao za uwanachama kwa
wakati ili kuwawezesha vijana wa watanzania kutimiza ndoto zao na kuigeuza
dunia kuwa wanachotaka. Kupitia klabu hii siyo lazima kuwa kila utakachochangia
lazima kikunufaishe, mchango wako utakuwezesha kuwa miongoni mwa wadau
watakoweza kunufaika na fursa ambazo michango yanu kama marafiki itakuwa
imetumika kuzitengeneza kupita vijana wetu wenye vipaji watakaokuwa makambini.
Ni wazi kuwa sasa wanachi wa mkoa wa Mbeya na watanzania
wangine wote tunapaswa kumuunga mkono mkuu wa mkoa Mh. Amosi Makalla, mkuu wa
wilaya na uongozi mzima
wa halmashauri ya wilaya ya Chunya, kwa kujiunga na klabu ya marafiki wa
Tanzanite City ili tuweze kushiriki kikamilifu kutengeneza fursa za kiuchumi
zitakauzo tufaidisha watanzania wote kwa maendeleo ya wote!
No comments:
Post a Comment