Maendeleo ya kitenolojia ni moja ya nguzo kuu muhimu sana
katika taifa katika kuongeza ufanisi wa uzalishaji, kupunguza upotevu na
kuongeza ubora wa bidhaa, pamoja na kuongeza ushindani katika sekta husika.
Jambo moja kubwa na la msingi katika kudumisha ushindani ni uwezo wa washindani
kubadilika haraka kuendana na mabadiliko ya mahitaji ya soko la kimataifa.
Tunaweza kuuelezea uwezo
wa taifa kiteknolojia katika ngazi kuu tatu ambazo ni: mosi ni uwezo wa kutunza
na kuendesha mitambo ya uzalishaji iliyonunuliwa toka ng’ambo; pili ni uwezo wa
kunakili au kukopi na kufanya marekebisho muhimu ili mitambo iliyonakiliwa
iweze kuendana na mahitaji na mazingira ya mahali inapotarajiwa kutumika; tatu
ni uwezo wa kubuni na kusanifu mitambo au mifumo ya uzalishaji na vifaa vya
uzalishaji.
Maendeleo hayo ya
teknolojia yanaongozwa na weledi wa kiubunifu katika uvumbuzi wa bidhaa mpya na
kuzifikisha sokoni. Ili kuweza kuwa na weledi wa ubunifu na namna ya kufikisha
sokoni bidhaa hizo mpya kunahitajika kufanyika kwa utafiti wa kina na majaribio
mengi ya kisayansi (experimentation), ujuzi, motisha na sapoti ya kitaasisi
kuweza kupeleka bidhaa sokoni. Pamoja na kuwa mfumo rasmi wa kujenga weledi
unalenga tafiti na ubunifu katika mfumo ulio rasmi zaidi, unahusisha pia
majaribio yanye msingi wa kimasoko na kimatumizi kwa lengo la kuelewa walaji
wanahitaji nini. Utengenezaji na upelekaji sokoni wa bidhaa hizo pia unaweza
kufanywa katika mifumo yote ulio rasmi na usio reasmi.
Namna
ambavyo teknolojia inaweza kuingizwa inchini
Kuna namna nyingi
ambazo taifa linaweza kuingiza teknolojia mpya toka nje ikiwa ni pamoja na
biashara za kawaida za uagizaji wa bidhaa za kiteknolojia toka nje nchi,
mikataba ya ruhusa ya kutumia kiteknolojia (licensing of technology); kuchangia
teknolojia (sharing of designs), haki miliki (patents), kanuni (formulae), ubia
kwenye miradi mikubwa ya teknolojia ya juu, (high-tech joint ventures);
kusomesha wataalam nje ya nchi; ushirikiano kwenye mambo ya msingi ya ubunifu
na uendaelezaji teknolojia (collaboration in basic and/or innovative research
and development); pamoja na misaada ya kiteknolojia (donated technologies,
machinery, or equipment). Vile vile kuna njia ambazo ni kinyume cha uungwana,
hizi pia zinaweza kuwa kupewa mamlaka ya
kuingiza teknolojia kwa kubadilishana na soko; kutumia teknolojia kinyume na
makubaliano ya msingi ya uingizaji wa teknolojia husika, wizi au kugushi
makabrasha ya teknolojia (theft or infringement of intellectual property) na
kuchunguza kwa siri teknolojia za wengine (espionage)
Lengo kuu na la msingi la
kuingiza teknolojia ni kupata manufaa ya kiuchumi (economic gain) iwe ni ya
muda mfupi au muda mrefu. Kwa ujumla hamasa kubwa ni (i) kuinginza nchini
teknolojia mhimu na sahihi ambazo hazipatikani ndani ya nchi, na (ii) kujenga
uwezo wa ndani kiteknolojia katika eneo mahususi au sekta kupitia uzalishaji,
uhandisi au ubunifu katika teknolojia zinazoingizwa nchini.
Serikari
na wadau ni lazima kuhimiza kuingizwa nchini kwa weledi/ujuzi na taarifa za
kisayansi na kiteknolojia kutoka nchi zilizoendelea, pia tuhimize umuhimu wa
kueneza na kuhakisha kuwa teknolojia zote zinazoingia nchini zinapelekea kukua
kwa teknolojia zetu na kuhama kutoka teknlojia za hali ya chini “low-tech”na kuelekea kwenye teknloljia za hali ya juu
“high-tech.” badala ya kuzalisha
vitu vidogovidogo kama mabatiki mishumaa sabuni n.k. tuanze kuzalisha vitu kama kompyuta, magari
simu za kisasa, meli, ndege n.k.
Ni lazima tuweke
mkazo mkubwa sana kwenye uwezeshaji wa wajasiliamali wetu wakubwa na wadogo ili
waweze kuzalisha bidhaa bora za kiteknolojia zitakazoweza kukushindana vilivyo
katika soko la ndani na la nje, hivyo kuongeza ajira na kukuza uchumi
Yatupasa sasa tujipange
kwa mikakati madhubuti ya kuhakisha kuwa wajasilia mali wetu wadogo na wakati
ndiyo wanakuwa kiini cha utafiti wa kiteknolojia na ubunifu wa bidhaa bora
kabisa, serikari na taasisi zake zijenge madaraja baina yao na wajasiliamali
wazalendo ili waweze kupata fursa ya kutumia miundo mbinu iliyopo nchini kwa
manufaa ya maendeleo ya taifa letu, ni lazima sasa tuwahamasishe wajasiliamali
wetu wa Tanzania kujikita katika kuzielewa na kuzitumia ipasavyo teknolojia
zinazoingia nchini badala ya kuangalia zaidi faida ya haraka haraka kutokana na
teknolojia zinzoingia hapa nchini, tujikite katiaka kuingiza nchini teknolojia
sahihi ambazo hazipatikani hapa kwetu na ambazo ni mwafaka kwa maendeleo yetu,
lakini pia tusisahau kusomesha vijana wngi zaidi na kuliandaa taifa kwa kuwa na
wafanyakazi wa kutosha wenye ujuzi na owezo wa kukabiliana na changamoto za
maendeleo ya teknolojia, tuwaanda vijana wetu kuwa wanasayansi wa kesho,
mafundi, madaktari n.k.
Ili tuweze kufaninikiwa
katika hili tunapaswa kufanya uwekezaji mkubwa kwenye teknolojia ili mwisho wa
siku vijana tutakaokuwa tumeasomesha wasije wakakosa sehemu za kuutumia weledi
na ujuszi wao, vilevile ni lazima tuwe na mkakati wa kuhakiksha wataalam wote
wenye vipaji maalum hawandoki nchini kwa kuwatengenezea mazingira bora ya wao
kutumia vipaji vyao kwa manufaa ya taifa huku na wao wakifaidika na matunda ya
juhudi zao jambo litakalowafanya waione haja ya kutimkia nje ya nchi mara tu
wanapomaliza masomo yao ya juu
Tujenge uwezo wa kuzielewa
na kuzitumia kwa ubunifu teknolojia zinazoingia nchini kwakuweka mkakati wa
makusudi wa kuwa saidia wajasiliamali wanashughulika na teknolojia kwa
kuwapunguzia urasimu wa kupata mikopo katika mabenki, taasisi za kutoa huduma
kama TFDA, TRA, Na kwingineko kama wanavyofanyiwa wawekzaji wa kigeni,
wasamehewe kodi ili viwanda vyao viwekeze zaidi kwenye utafiti na maendeleo ya
teknolojia, wapewe rasilimali ambazo haziligharimu chochote taifa kama vila
ardhi bila masharti makubwa ili iwasaidie katika kukua na kuwekeza, kama hayo
yanawezekana kwa wgeni sioni kwanini yashindikane kwa wananchi wetu wenyewe,
serikari itenge kila wilaya nchini eneo maalum la ardhi kwa ajili ya uwekezaji
wa ndani wa wajasiliamali katika teknolojia, walau kila mkoa uwe na kituo
kikubwa cha kiashara “business park” ambapo wajasiliamali watauzia bidhaa zao
na kuwa kama sehemu ya maonyesho ya kitknolojia na kuwakutanisha wajasiliamali
mbalimbali na wateja wao na kuwa kitua cha taarifa za kisayansi na teknolojia
Mikiakati yetu ni lazima ilenge katika
kuwa na viwanda vingi vidogovidogo vya uzalishaji bidhaa mbalimbali kuanzia
vifaa vidogovidogo vya elektroniki hadi kompyuta za hali ya juu kabisa,
teknolojia ya habari, usafiri wa anga, maji na barabara. Tupo nyuma lakini
hatujachelewa, tuanze sasa tutafika tu!!!
No comments:
Post a Comment