DHUMUNI KUU
Tanzanite City ni jiji la sayansi, teknolojia na ubunifu ambalo
lipo njiani kujengwa mkoani Mbeya katka wilaya ya Chunya. Jiji hili linajengwa kwa ushirikiano kati ya ESTA-TZ na ofisi ya mkuu wa mkoa, Mh. Amos Makalla, ofisi
ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mkurugenzi na Balaza la Madiwani wa Halmashauri ya
wilaya ya Chunya.
Lengo kuu la kuanzishwa kwa
Tanzanite City ni kujenga uwezo wa taifa letu kwenye mambo ya teknolojia na
kuhamasisha mapinduzi ya viwanda yatakayoifanya Tanzania kuwa kiwanda cha
Afrika na kitovu cha ubunifu katika ukanda huu wa Afrika kusini mwa jangwa la
Sahara.
Jiji hili litasaidia kuwajengea uwezo wa ubunifu katika maswala
teknolojia, vijana wanaomaliza vyuo katika fani za sayansi na teknolojia, na
kuwawezesha kuanzisha viwanda na kuunda makampuni watakayo yaendesha kwa ubia
na wanachi wengine, kupitia klabu ya marafiki wa Tanzanite City
BAADHI YA CHANGAMOTO TUNAZOKWENDA KUZIJIBU
Kama
tujuavyo serikali yaawamu ya tano ya Mh.
John Pombe Magufuli imedhamiria kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa viwanda,
Lakini katika safari hiyo kuna changamoto kadhaa ambazo ni lazima zifanyiwe kazi.
· Mazingira magumu na
yasiyo rafiki yanayoyoua utamaduni wa kuwekeza katika
viwanda yanawafanya watanzania wengi kuagiza bidhaa za viwanda toka nje,
· Kukosekana kwa
kiunganishi kati ya wanjasiriamali wazawa na wawekezaji wa nje kunakotokana na tofauti kubwa sana katika technoljia. Tofauti hii
imefanya kuwa vigumu sana kwa wazawa kuweza kuhamisha teknolojia toka ng’ambo
hivyo kudumaza kabisa uwezo wetu na kutufanya tuendelee kuwa tegemezi
· Kukosekana kwa
mikakati sahihi ya kukuza na kuendeleza teknolojia ambayo
imefanya Kushindwa kubadli mafanikio ya tafiti kuwa viwanda (industrialization
of applied research); kushindwa kugeuza viwanda kuwa fursa za kibishara ambako
ndiko pesa ilipo.
SULUHISHO LETU
Ili
kujibu changamoto hizo, jiji la Tanzanite City limeanzishiwa kwa lengo la
kuweka mazingira bora ya kukuzwa ubunifu na kuanzishwa kwa viwanda na
makampuni. MAMBO SITA MUHIMU YATAKAYOFANYWA
NA TANZANITE CITY
1. Miundombinu bora (infrastructures
and sound facilities)
2.
Mikakati mahususi ya kukuza
vipaji na ubunifu
3.
Upatikanaji wa mitaji na
fedha
4.
Upatikanaji wa huduma
mbalimbali
5.
Kujenga mfumo madhubuti wa
biashara (Adequate business systems);
6.
Kutangaza na kukuza taasisi
za wajasiliamali na ujasiliamali (Promotion of SMIEs and entrepreneurship);
JIJI LITAKAVYOFANYA KAZI
Watu
wenye vipaji toka kokote kule duniani wataalikwa kushirikiana na vijana wetu
wataalam katika fani za Sayansi na teknolojia wanaohitimu vyuo ambao watawekwa
kwenye makambi ya teknlojia (classified technology development camps), katika jiji hili ili waweze kubuni na kujenga
uwezo wa kutengeneza bidhaa mbalimbali za kitechnolojia huku wakipewa kila aina
ya msaada watakaohitaji, kuanzisha viwanda pamoja na kuanzisha makampuni
watakayoyamiliki kwa ushirika na watanzania wengine kupititia Klabu ya marafiki
wa Tanzanite City.
Vijana hawa wataalam
watapewa mission mahususi za kubuni na kujenga uweza wa kuzalisha teknlojia
kulingana na vipaumbele na mahitaji soko, kukopi teknolojia ambazo tayari zipo,
kuzifanyia maboresho kulingana na mahitaji ya soko, na kuanzisha bidhaa na
teknoljia mpya ambazo ni zetu wenyewe baada ya kuwa tumejenga uwezo wa kutosha.
Lengo ni kujenga
uwezo wetu wa ndani wa kuzalisha bidhaa za kiviwanda na kiteknoljia, kwa mfano
badala ya kuuza simu toka nchi za Asia, tuunda na kuuza simu zetu wenyewe!
Badala ya kuifuata Guangzhou kule Uchina tunataka kujenga Guangzhou yetu hapa
hapa nchini
TUNAHITAJI NINI TOKA KWAKO MDAU
Tunawataka
wanachi na wadau wengine kujiunga na
klabu ili;
Kwanza waweze
kuchangia kwenye ujenzi wa jiji kwa
fedha au mawazo
Pili waweze kushiriki
kikamilifu kwenye ujenzi wa Tanzania mpya
Wewe kama mdau muhimu
tunakuaomba tuungane na Mh Rais John Pombe Magufuli na mkuu wetu wa Mkoa ambaye
pamoja , Wabunge wetu katkia juhudi zao za kuleta maendeleo ya Viwanda na
kukuza uchumi wa Mkoa wetu .
TUMEDHARIA
KUIFANYA MBEYA KUWA GUANGZHOU YA AFRIKA,