Wazo la kuanzishwa kwa Tanzanite City limetokana na tafiti nyingi
tulizozifanya kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi iliyopita. Tafiti hizo
zililenga kutufanya tujue wenzetu waliokuwa
na ndoto kama zetu walipitia changamoto zipi, na kama waliweza kufaulu
walifanya nini cha tofauti na kama walifeli walikosea wapi. Vilevile tulilenga kutambua mifumo na mikakati sahihi ya kufuata
ili kuweza kuwa na mafanikio tunayohitaji kuifikia Tanzania ya viwanda. Mambo yafuatayo tuliyazingatia kwenye tafiti zetu:
a.
Tuliangalia
matarajio na mwenendo wa masuala ya teknolojia na ubunifu pamoja na mabadiliko
katika uchumi wa dunia
b.
Historia na
uzoefu wetu hapa nyumbani na wa mataifa mengine katika masuala ya sayansi na
teknolojia pamoja na maendeleo ya kitaasisi.
c.
Tuliangalia
hali halisi ya sasa, uwezo na rasilimali tulizonazo, miundo ya kitaasisi na
mikakati yetu kama taifa
d.
Tukafanya
upembuzi wa mafanikio na matatizo/changamoto ambazo mataifa mengine yaliyokuwa
na malengo kama yetu walipitia katika kufikia malengo yao.
Tafiti hizo zilituonyesha kuwa, iwapo tutatengeneza mazingira hamasishi
kwa shughuli za utafiti na ubunifu pamoja na kuwezesha uanzishaji wa makampuni
kwa utaratibu rahisi na rafiki kisha kuwavutia wawekezaji wa nje kuingia ubia
na watanzania, Tanzania inaweza kabisa kupiga hatua kubwa katika mapinduzi ya
teknolojia na viwanda sawa kabisa na mataifa mengine yote yaliyoendelea ikiwamo
Uchina, india, Indonesia, Malaysia n.k.
Kwa hiyo mchakato wa ujenzi wa Tanzanite city unatokana na uzoefu
tulioupata kutoka kwa mataifa ambayo yamefanikiwa kupata maendeleo makubwa ya
kiteknolojia na kiviwanda katika miongo michache iliyopita. Swala la msingi ni
kuhakikisha kuwa mchakato mzima unaendana na hali halisi na changamoto mahsusi
za taifa letu na mazingira yaliyopo. Vile vile, mchakato mzima lazima ujikite
katika mipango halisi na inayotekelezeka.
Ili kuweza kukidhi mahitaji ya kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa
viwanda, uanzishwaji wa jiji la Tanzanite City umezingatia mambo yafuatayo
ambayo ni ya msingi:
a.
Mkakati
mahususi (Focused strategy); mkakati mahsusi wa ujenzi wa Tanzanite City ni
kujenga na kuimarisha uwezo wetu wa ndani wa kubuni teknolojia na kuanzisha
viwanda pamoja na makampuni ya teknolojia. Kuwashirikisha watanzania wazawa
kupitia klabu ya marafiki wa Tanzanite City kumiliki viwanda na makampuni
badala ya kubaki watazamaji tu ndani ya nchi yao.
b.
Miundombinu
inayokidhi haja maridhawa (Sound facilities & infrastructures); ujenzi wa
miundombinu muhimu utawanufaisha wanasayansi na wabunifu wetu kwa kuwawezesha
kufanya tafiti zao kwa uhakika na kujiamini.
c.
Kujenga mfumo
madhubuti wa biashara (Adequate business systems); mfumo madhubuti wa
kibiashara utarahisisha upatikanaji wa huduma muhimu na kuvutia wawekezaji,
wafanyabiashara na wajasilamali pamoja na wataalam mbalimbali katika fani zote
kuja kuwekeza rasilimali zao Tanzanite City.
d.
Ukuzaji wa
teknolojia na vipaji (Development of talents and technology); kukuza vipaji na
uendelezaji wa teknolojia kwa kuwajengea uwezo vijana wanaomaliza katika
taasisi zetu za elimu ya juu na kuwawezesha kubuni teknolojia na vifaa vya
uzalishaji pamoja na kuwasaidia kujenga viwanda na kuanzisha makampuni.
e.
Kuwezesha
upatikanaji wa mitaji na fedha (Access to capital and financing); moja ya
matatizo makubwa ya wajasiliamali na wataalam wa teknolojia hapa nchini ni
upatikanaji mgumu wa mitaji na fedha za kugharimia tafiti na kubunifu.
Tanzanite City ina mkakati wa makusudi wa kuhakikisha kuna upatikanaji wa
uhakika wa fedha za mitaji na kuendeshea tafiti mbalimbali. Lengo ni kuwafanya
wataalam wetu wazingatie zaidi shughuli za kitafiti badala ya kufikiria namna
ya kupata pesa kwa ajili ya kuendesha maisha pamoja na kujikimu wao wenyewe.
f.
Kusaidia
kupromoti taasisi za wajasiliamali na ujasiliamali (Promotion of SMIEs and
entrepreneurship); baada ya wataalam wetu kubuni teknlolojia na bidhaa zao kwa
ufanisi, kujenga uwezo wa kuzalisha kwa wingi na kwa viwango vya kimataifa, kitakachofuata
ni kuwasaidia kujenga viwanda na kuanzisha makampuni watakayo yamiliki kwa ubia
na watanzania wengine kupitia klabu ya marafiki wa Tanzanite City. Makampuni
haya ndiyo yatakayo tengeneza fursa za kibiashara ambazo ndizo zitakazowaletea
fedha pamoja na kujenga mahusiano baina
ya watanzania na wawekezaji wa kigeni katika masuala ya teknlolojia na viwanda
MTANZANIA
MWENZANGU UKIONA JAMBO HALIJAFANYIKA, JUA NI MIMI NA WEWE HATUJALIFANYA. ACHA
LAWAMA NA UCHUKUE HATUA; JIUNGE NA KLABU YA MARAFIKI WA TANZANITE CITY USHIRIKI
KUIJENGA TANZANIA MPYA YA VIWANDA KUPITIA TANZANITE CITY!
Kwa
maelezo zaidi tembelea - https://esta-tanzanitecity.blogspot.com/p/friends-club-of-tanzanite-city.html
Katika
sehemu itakayofuata (Tanzanite City - Part 03) tutazungumzia Klabu ya Marafiki wa
Tanzanite City; nini lengo la kuanzishwa kwake, kwa nini ni muhimu ujiunge na
klabu, fursa na faida za kuwa mwanachama au rafiki wa Tanzanite city n.k. TWENDE
PAMOJA HADI KIELEWEKE!